Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Privacy Policy

Sera ya Faragha ya Mabadiliko Forums.

Ulindaji wa Taarifa:

Mabadiliko Forum, itajiendesha kwa kuzingatia misingi ya Faragha ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za wanachama na wale wanaotembelea Wavuti hii. Italinda Taarifa binafsi za wanaojisajili, na katika kufanikisha hayo itazingatia kanuni na misingi ya sheria ya Kimataifa zinazohusiana na masuala ya Mitandao.

Kushiriki Mijadala ndani ya Wavuti: Ili kutoa habari na kuchangia mijadala katika Wavuti ya Mabadiliko Forum hii ni lazima kujiandikisha, ambapo utapaswa kutoa taarifa binafsi za kukubainisha wewe. Katika taarifa hizo binafsi utapaswa kujiandikisha kwa Jina lako kamili (ni lazima jina liwe halisi), Mahali ulipo (Location) tarehe yako ya kuzaliwa (muhimu kujaza tarehe halisi) kwani pia itasaidia wakati wa kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa kwako na kuweka Picha yako halisi.

Kutumia Anwani ya Barua Pepe (Email): Kila anayejisajili atapaswa kutumia Anwani sahihi ya Barua Pepe ambayo itamsaidia kuwasiliana na Uongozi na Utawala wa Wavuti na hata wakati atakaposahau ama kupoteza Nywila (Password) yake hivyo kuwa rahisi tumiwa ujumbe binafsi kwenye Email yake kwa msaada.

Ukusanyaji wa habari:

Habari zozote zitakazoandikwa zitakuwa ni za mtu binafsi na siyo za wavuti hii, lakini katika kuhakikisha tunakuwa na habari bora zaidi inaweza kuzuiliwa kutoka ama kuondolewa kwa lengo la kuichunguza, kuiboresha ili kuifanya kuwa bora zaidi kwa ajili ya kutoa taarifa za uhakika.

Utoaji wa Huduma:

Wavuti yetu, inaweza kutumika kama chanzo cha Habari na utoaji wa huduma nyingine kama sehemu ya tovuti yetu (mfano, uuzaji wa bidhaa na ununuaji, Huduma za fedha, Hali ya hewa, Habari, Mashindano, Bahati nasibu na Matangazo).

Utoaji taarifa za Uhalifu:

Uongozi wa Wavuti hii, tunayo haki ya kutoa taarifa binafsi za mtu wakati zinapohitajika iwapo anadaiwa kufanya mambo kinyume cha sheria ama wakati wa mchakato wa kisheria, pia kushirikiana na wachunguzi wa masuala ya makosa ya Jinai (makosa makubwa), kwa kutambua watu kukiuka sheria.

Faragha ya watoto:

Mabadiliko.com inajali na kulinda usalama wa watoto katika matumizi ya mtandao. Kwa hiyo, kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi ya Faragha ya Watoto ya 1998, hatutaweza kumsajili mtu mwenye chini ya  Umri wa miaka 18 bila ridhaa na uthibitisho wa Wazazi wake. Na iwapo itatokea kuwapo kwa taarifa za kusajiliwa kwa mtu ambaye yupo chini ya umri huo, bila idhini na uthibitisho wa wazazi, hatua za kumfuta kutoka kwenye kumbukumbu zetu itafanyika haraka.

Iwapo kama una maswali kuhusu sera yetu na Mahudhui ya Jukwaa hili la Mtandao wa Mabadiliko.com, tafadhali wasiliana na;

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwanza, Tanzania

Add comment


Security code


Refresh