Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Matokeo ya David Kafulila, Hasna yahairishwa kutangazwa

KafulilaKIGOMA: Matokeo ya Jimbo la Kigoma Kusini yamezua utata hivyo kumlazimu msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo kulazimika kuwasiliana na mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi naye kuagiza kusitisha zoezi la utangazaji wa matokeo.

Akielezea maagizo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Kusini, Reuben Fuime amesema wamelazimika kusitisha utangazaji wa matokeo ya jimbo hilo kutokana na mgombea wa CCM Hasn Mwilima kugomea matokeo baada ya zoezi la kuhakiki kukamilika.

Alisema walilazimika kusitisha zoezi hilo jana saa 4:15 usiku na kuwasiliana na makao mkurugenzi wa tume wa Taifa makao makuu na kupewa maelekezo kusitisha matokeo hayo mpaka hapo watakapopata maelekezo kutoka makao makuu ya tume.

Akizungumza na waandishi baada ya msimamizi wa Uchaguzi, David Kafulila (NCCR Mageuzi) alisema amgomea ombo la mgombea wa CCM la kutaka waanze upya zoezi la kurejea kuhesabu upya kura zoto kutoka katika masanduku kwa madai kuwa kura hizo zimelala hapo na upo uwezekano kuwa zilichezewa usiku.

“Matokeo yamebandikwa katika kata na vituo wamehesabu na kukubaliana, sasa anataka tuanze kufungua masanduku na kuhesabu upya nimegoma na hilo ndilo limeababisha msimamizi wa uchaguzi kushindwa kutangaza na kuwasiliana na tume na kutoa tangazo hilo,” alisema.

Wakati mkurugenzi akitangaza hayo wananchi wafuasi wa vyama vyote walikuwa wamekusanyika katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza wakingoja matokeo huku upande wa wafuasi wa NCCR wakishangilia sawa na wale wa CCM. Kutokana na hali hiyo Polisi waliimarisha ulinzi katika ofisi hizo kwa hofu ya kuzuka vurugu.

Wagombea wengine katika jimbo hilo ni Bakema Rashid (ACT), Bidyanguze William (ADA TADEA) pamoja na Sala Michael Ntahiye (DP) lakini ushindani mkubwa ulikuwa baina ya David Kafulila wa NCCR na Hasna wa CCM ambao wamesababisha kuhairishwa utangazaji wa matokeo hayo.

Add comment


Security code


Refresh