Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Ubunge Nyamagana, Wenje kupinga Mahakamani

Wenje akiwa katika KampeniMWANZA: Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Nyamagana umezua kizaa ambapo aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Ezekiel Wenje (CHADEMA) ametangaza kuyapinga matokeo yake mahakamani.

Akizungumza na jana na waandishi wa habari katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, Wenje alisema anakusudia kufungua shauri hilo kutokana na mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula kutangazwa kwa nguvu kuwa mshindi.

Alisema matokeo yaliyotangazwa na yale waliyoyapata baada ya kurudia kufanya majumuisho kutoka kata mbalimbali za jimbo yalitofautiana sana na hayakuandikwa katika karatasi zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kwenda kutangazwa.

“Baada ya kupitia matokeo kutoka kata zote na nakala ambazo zilisainiwa na mawakala wa CCM pia na kufanya majumuisho tulikubaliana tuyarudufu (printing) ndipo atangazwe mshindi lakini nikashangaa hawataki kukubaliana na mimi na wakaamua kumtangaza Mabula kwa matokeo tofauti na matokeo halisi,” alisema Wenje.

Alisema wiki mbili kabla ya uchaguzi Mkurugenzi wa jiji la Mwanza,  Halifa Hilda alihamishwa kituo cha kazi kitu ambacho ni kinyume cha sheria na taratibu za uchaguzi ambazo zinakataza msimamizi wa uchaguzi wa jimbo kuhamishwa siku chache kabla ya uchaguzi na kama italazimu kuhamishwa ni vyema wakawasiliana na tume.

alisema mbali na mpango wa kuhujumu matokeo, sababu zingine za Hida kuhamishwa ziliztokana na kukataa kutoa fedha za halmashauri zitumike katika kampeni na mipango ya CCM ya kuandaa ushindi ikiwa pamoja na  msimamo wake wa kumtangaza atakayekuwa mshindi halali wa ubunge jimbo la Nyamagana.

Wenje amelalamikia pia kukiukwa kwa kiasi kikubwa kwa sheria ya uchaguzi inayotaka matokeo ya urais katika kituo kuandikwa kwenye fomu namba 21 A, ubunge 21B na udiwani 21C ambapo katika kata nyingi mawaWenje akionyesha nyaraka za uchaguzikala wa vyama vya siasa walinyimwa fomu hizo na kulazimika kujaza matokeo hayo katika karatasi za kawaida  zilizogongwa muhuri wa tume ya uchaguzi.

Akitangaza matokeo ya Jimbo hilo juzi usiku majira ya saa 6:50 usiku, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana, Tito Mahinya alisema mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula alishinda kwa kupata kura 81,017 dhidi ya mpinzani wake Wenje, aliyepata kura 79,280.

Alisema jimbo hilo lilikuwa na wagombea saba ambapo wagombea wengine walikuwa ni Chacha Okong’o,  ACT Wazalendo aliyepata kura 161, Faida Hassan Potea (CUF) aliyepata kura 1,005, Mohamed Msanya, (Jahazi Asilia) aliyepata kura 175, Mohamed Mkangwa, (NRA) kura 104 na Ramadhan Mtoro wa UDP yeye aliambulia kura 68.

Matokeo hayo yalichelewa kutangazwa kutokana na kuwepo kwa mabishano baina ya Wenje na Mabula hatua ambayo ilizua hofu na kusababisha wasiwasi kiasi cha kuwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mwanza kuwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiusanyika maeneo mbalimbali.

Awali matokeo yalitarajiwa kutangazwa saa 3.00 asubuhi juzi, lakini walitaarifiwa kuwa yatatangazwa mchana saa 7 lakini mpaka muda huo walidai kuanza zoezi la kuhakiki upya matokeo hayo.

Viongozi wa CCM watinga Jiji:

Zoezi hilo la uhakiki wa kila kata na vituo lilichukua muda ambapo mpaka saa 4.38 usiku lilikuwa likiendelea ambapo viongozi wa CCM (Katibu wa Mkoa wa Mwanza) Miraji Mtaturu akiwa ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Sharif Mansoor (Mweka hazina wa CCM), walifika katika ofisi za Jiji na kuingia ndani.

Baada ya muda mfupi majira ya saa 5:20 usiku Katibu alitoka na kuomba kuongea na kituo cha Azam Televisheni ambacho kilikuwa kikirusha matangazo ya moja kwa moja na kusema waliamua kufika ofisi za Tume kwa ajili ya kufahamu kilichokuwa kikikwamisha utangazaji wa matokeo hayo.

“Kama mtu ameshindwa akubali matokeo na siyo kusumbua watu tangu asubuhi wananchi wanasubiri matokeo halafu mtu mmoja tu anakwamisha huku ajijitengenezea mazingira ya kuandaa vijana wafanye fujo. Tumemuuliza msimamizi wa uchaguzi amesema atatangaza muda mfupi kuanzia sasa, tunataka atangaze ili zoezi hili liishe hakuna sababu ya mtu mmoja kusumbua watu kwa kutaka warudie kura,”alisema.

Wenje azungumza na waandishi:

Ilipofika saa 6.41 usiku Wenje alitoka nje ya chumba cha majumuisho ya kura na kueleza kuwa ameshinda lakini msimamizi wa uchaguzi amelazimisha kumtangaza mgombea wa CCM kuwa ndiye mshindi kutokana na shinikizo alilolipata toka kwa viongozi wa juu akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.

“Demokrasi inabakwa hapa nchini, sijasaini maana sijaridhika na matokeo na nitashauriana na viongozi wangu wa chama kuona tunafanya nini ila lazima tutafute haki..., msimamizi amelazimisha kumtangaza mgombea wa CCM ambaye nimemshinda kwa kura nyingi kwamba ndiye mshindi, tumefanya excel kituo kwa kituo tangu asubuhi ndiyo maana tumeshinda hapa hadi muda huu.

“Mimi  nimepata kura 85,039 mgombea wa CCM amepata kura 82,000 lakini  amefungua kitu walichokwisha tengeneza akamtangaza,”alisema.

Usiku huo wakati wakitangaza Jesho la polisi lilikuwa likipiga mabomu ya machozi katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza usiku hali ambayo ilielezwa na kamanda wa Polisi Mkoa kuwa walikuwa wakitawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakikusanyika.

Mabula azungumza:

Baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi wa jimbo la Nyamagana, Mabula alisema anawashukuru wananyamagana kwa kufanya mabadiliko yaa kweli na kuichagua CCM hivyo wategemee kubadiliko ya maendeleo ndani ya jimbo hilo huku akiahidi kujitoa kwa nguvu zake zote kuwatatulia kero wananchi wa jimbo lake.

Add comment


Security code


Refresh