Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Tamunet yafanikisha Bima ya Afya: Sasa wanamuziki kupatiwa Matibabu

Mwanamuziki MbutuDAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), John Kitime amewashauri wapenzi wa wanamuziki nchini kuwasaidia kulipia Sh 76,800 kwa mwaka ili waweze kupata Bima ya Afya kuliko kumchangia fedha za matibabu ya muda mfupi pale wanapougua na kuzidiwa.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi Vitambulisho vya Bima ya Afya kwa wanamuziki ambao tayari wamekamilisha mchakato wa kujiunga, alisema kukamilika kwa mpango huu kunatokana na maazimio ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Muziki Duniani (FIM).

Kitime alisema katika mkutano huo wa mwaka 2004, moja ya maazimio ya mkutano ule ilikuwa kila nchi ihakikishe inaanzisha utaratibu wa Bima ya Afya kwa wanamuziki wake hivyo alianza harakati hizo na mara baada ya kurudi nchini kufanikiwa sasa.

“Mara baada ya kurudi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa TAMUNET, tulianza kufuatilia uwezekano wa kupata huduma ya Bima hiyo kwa wanamuziki, bahati mbaya hakukuwa na njia yenye gharama nafuu ya malipo ya Bima hiyo ambayo mwanamuziki wa kawaida angeweza kuimudu. Kulikuwa na kampuni ambayo iliweza kutoa huduma hiyo kwa gharama ya dola 300 kwa mwaka kwa mwanamuziki mmoja.

“Kampuni nyingine za Bima zilizotembelewa hazi kuonyesha ushirikiano katika jambo hilo na ndipo TAMUNET iliwasiliana na mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa katika kipindi hicho mfuko ulikuwa hauna mamlaka ya kuhudumia watu waliokuwa nje ya ajira ya serikali na mashirika ya umma,” alisema.

Kutokana na hali hiyo mpango huo ulishindikana mpaka mwaka 2015 ndipo mlango ulifunguka kwa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ulipoanzisha mpango wa Bima kwa kikoa ambao ungewawezesha wanamuziki nao kupata Bima ya Afya kwa gharama nafuu.

Kitime alisema katika mpango huo wanachama wa TAMUNET ambao ni wananamuziki wanapaswa kulipia Sh 76,800 kwa mwaka na kuwataja wanamuziki ambao tayari wamejiunga na bima ya afya chini ya mpango huu kuwa ni Louiza Nyoni, Abdul Salvador, Rashid Pembe.

Mpango huu utaondoa aibu ya wanamuziki kuchangiwa fedha za matibabu kila wanapougua jambo ambalo limekuwa likiwatia aibu hivyo kuwahimiza wanamuziki kuchangamkia fursa hiyo kwa faida yao.

Add comment


Security code


Refresh