Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Kituo cha aliyekuwa Kocha Stars: Silvester Marsh chapokea rambirambi

StarsMWANZA: Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza imetoa rambirambi zake kwa msiba wa aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa Stars, Silvester Marsh aliyefariki machi 14 mwaka huu baada ya kuugua maradhi yake ya Saratani ya Koo.

Rambirambi hiyo imekabidhiwa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa Kituo cha Kukuza na Kuibua Vipaji cha Marsh Athletic cha jijii Mwanza na kubainisha kuwa rambirambi hiyo ni sehemu ya awadi waliyoitoa wakati wa msiba wake.
 
Akizungumza na BINGWA juzi, Msemaji wa Kituo hicho Steven Buyuya, alisema rambi rambi waliyopokea ni Sh 500,000 na kutumia nafasi hiyo kuwakumbusha wadau wengine ambao walihaidi kutoa na hawakutoa.
 
Alisema kupokea rambirambi hiyo kumewafariji kwa kuwa imefika wakati ambao inahitaji kuendeleza kituo hicho ambacho kiliachwa na Kocha Marsh.
“Tumepokea fedha hizo kutoka CCM, tunaona na wengine walioahidi wajitokeze kukamilisha ahadi zao ili kukusaidia kituo chetu ambacho sasa hivi kinajiendesha chenyewe kutokana muasiasi wake kufariki dunia,’’ alisema Buyuya.
 
Hata hivyo aliwaomba wapenzi na mashabiki wa timu ya Marsh wajitokeze kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa moyo na nguvu wachezaji ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo yake ikiwemo mashindano ya Airtel Rising alisema.

Add comment


Security code


Refresh