Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

Mgodi wa GGM watoa Sh milioni 300: Wadhamini timu ya Geita Gold Sport

Hundi ikikabidhiwaGEITA: Timu ya mpira wa miguu ya Geita Gold Sport ya mkoani Geita inayoshiriki ligi daraja la kwanza  imepata udhamini mnono wa Sh milioni 300 kutoka Mgodi wa Dhabu wa Geita (GGM).

GGM imesaini mkataba rasmi na timu hiyo kama fedha za kuifadhili timu hiyo katika michuano yake ya kuwania ubingwa wa daraja la kwanza itakayoanza mwezi Septemba mwaka huu 2015/16.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi cheki hiyo, Meneja wa Mgodi wa Geita Terry Mulpeter alisema GGM inajivunia kushiriki katika ufadhili wa timu  hiyo.

“Ufadhili huu  ni zaidi ya fedha tunazotoa, ni  uboreshaji wa mahusiano katika jamii  yetu na uhamasishaji wa mazoezi kwa ajili ya afya bora za wanajamii wanaozunguka mgodi wa geita, hivyo GGM itakuwa bega kwa began na timu hii ili kuitangaza Geita kupitia soka ndani na nje ya Tanzania hususani kwetu Uingereza,’’alisema Terry  Mulpeter.

Uongozi wa timu ya Geita gold umetoa pongezi kwa ufadhili wa fedha hizo ambazo zitatumika katika utoaji wa posho, usafiri wa wachezaji na malazi wakati wakiwa kwenye ligi, ambapo timu hiyo ina jumla ya wachezaji 30 katika msimu huu.

“Ufadhili wa GGM kwenye timu yetu utapata  nguvu ya ushiriki kwenye ligi hii yenye ushindani mkubwa kuliko hata ligi kuu…tunatambua kwamba ggm imekuwa ikifadhili timu hii huko nyuma lakini kwa ufadhili wa mwaka huu tunatarajia kushinda kombe hapo mwakani,’’alisema Mwenyekiti msaidizi wa timu hiyo Ally Twisti.

GGM imejikita katika ufadhili wa shughuli zinazoleta chachu za maendeleo katika jamii ikiwa ni pamoja na michezo, ambapo uongozi wa mgodi huo unatambua kwamba michezo ni kiunganishi muhimu katika kujenga mahusiano.

Add comment


Security code


Refresh