Mabadiliko Forums

Log in Register

Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *

DISCLAIMER AND RULES OF MABADILIKO FORUMS

AINISHO YA MARUFUKU NA KANUNI ZA MABADILIKO FORUMS

JUKWAA LA MABADILIKO (Mabadiliko Forum) ni Mtandao wa Kijamii wa bure nchini Tanzania, unaojiendesha kwa kanuni na utaratibu.

Kanuni na marufuku zifuatazo, ndizo zinazoongoza majadiliano katika Jukwaa hili la Mabadiliko linalopatikana katika wavuti za WWW.MABADILIKO.COM ama WWW.MABADILIKO.CO.TZ.

Tafadhali soma kwa makini kabla ya kujisajili na uzingatie kanuni hizi mara baada ya kukubaliwa kuwa mwanachama ndani ya Jukwaa. Kanuni hizo ni zifuatazo;

 1. Ili kusajiliwa Mabadiliko utatakiwa kutumia jina lako kamili na halisi, na kuweka Email halisi inayotumika pamoja na picha yako halisi.

 2. Kila mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anayo haki ya kujiunga na Jukwaa hili na kuasajiliwa kwenye rejesta ya Mabadiliko.
 3. Kila aliyesajiliwa ana haki na uhuru wa kuchangia ama kuanzisha mada ikiwa ni pamoja na kutoa mawazo yake, hivyo kwa kuzingatia uhuru huo ni lazima;
  3.(a). Mawazo yake yaheshimike/yaheshimiwe na kuthaminiwa
 4. Majadiliano yaendeshwe kwa Uhuru bila kuzuia haki ya mchangiaji kutoa mawazo yake.
 5. Haitaruhusiwa kutoa taarifa za uongo, zisizo thibitika.
 6. Habari kutoka mitandao/vyombo vingine vya habari ni lazima itaje chanzo (Source) husika.
 7. Jukwaa halitaegemea kwenye itikadi yeyote ya kisiasa wala dini, hivyo mijadala ya siasa ama dini italenga kuleta mabadiliko katika jamii.
 8. Mchangiaji hatoruhusiwa kutumia lugha yenye matusi, ubaguzi wa rangi ama jinsia, lugha yenye kukera, kuudhi  ama kuchefua na kukejeli wengine.  Pia ni kosa kuchapisha au kusambaza picha za utupu, kutishia wengine na kutetea shughuli haramu au kujadili shughuli haramu kwa nia ya kufanya nayo kazi. Lakini utani kama sehemu ya utamaduni wetu hautachukuliwa kama ni kejeli kwa mtu mwigine.
 9. Jukwaani kutaruhusiwa Matangazo madogo ya biashara ambayo yatawekwa na wanachama lakini matangazo makubwa yatalipiwa kusaidia gharama za uedeshaji Jukwaa.
 10. Michango ya Mijadala ilenge Mada husika inayojieleza katika kichwa cha habari cha Mada husika, mijadala mipya ianzishwe chini ya kichwa cha habari kipya.
 11. Sheria na taratibu zingine Universal zinazoongoza majukwaa yote ya mitandao duniani itazingatiwa pia.
 12. Ujumbe binafsi utumwe kwa njia ya Ujumbe Binafsi (PM) ama Email ya mhusika na usiwe sehemu ya majadiliano, ukiweka sehemu ya Majadiliano utakuwa mada hivyo hatutahusika na lolote.
 13. Kila mtu anahaki ya kujitoa/ kujiondoa mwenyewe kwa hiyari yake ama kwa kuondolewa na Uongozi na usimamizi wa Jukwaa hili iwapo ataonekana ameshindwa kuheshimu kanuni hizi.

Tafadhali kumbuka kuwa anwani zote (IP Adress) na kumbukumbu za wachangiaji Jukwaani zinatunzwa pamoja na majadiliano yote yanayofanyika Jukwaani.

Hivyo Uongozi wa Mabadiliko Forums hautahusika na mapungufu ya aina yoyote kwa maudhui yoyote yaliyowasilishwa na wachangiaji kwenye jukwaa hili hivyo jukumu la usahihi wa maoni ya washiriki linabaki kuwa lake mshiriki na hakuna dhima ya kisheria kwa ajili ya matokeo ya majadiliano.

Kila anayechangia anawajibu wa kuhakikisha kwamba kila anachoweka Jukwaani (maandishi, picha, video ama maudhui mengineyo) hayakiuki au kuvunja sheria ya hati miliki, biashara za watu, au haki binafsi.

Uongozi na wasimamizi wa MABADILIKO FORUMS wanaweza kufuta ujumbe woyote ambao wataamini hauzingatia kanuni na maudhui. Na iwapo utaguswa, kuchukizwa ama kukerwa na mada yoyote, tafadhali wasiliana na wasimamizi wa jukwaa hili; 

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwanza, Tanzania

Add comment


Security code


Refresh